Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) na Afisa Masoko na Mauzo TTCL Bw. Peter Ngota (kushoto) wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kuweka mtandao mmoja wa mawasiliano Serikalini hivi karibuni jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) akibadilishana Mkataba waliosaini  Mkurugenzi wa Kampuni ya Softnet Gilbert Herman (kushoto)  jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi akiongea na washiriki (hawapo pichani) waliohudhria hafla ya kusaini mikataba ya kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali hivi  jijini Dar es salaam
Mtendaji Mkuu Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari (kushoto) akiwapongeza makampuni ya Kitanzania  ya TTCL na Sosftnet  kwa kushinda zabuni ya kujenga mtandao wa mawasiliano na kuyashinda kampuni nyingine duniani. Kulia kwake ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria hafla ya kusaini mikataba ya kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali kati ya hivi karibuni jijini Dar es salaam.Picha zote na Eliuteri Mangi
---
Na Eleuteri Mangi Serikali imetiliana saini makubaliano na makampuni yaliyoshinda zabuni ya kujenga mtandao wa mawasiliano. 
 Makubaliano hayo yalisainiwa  jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi kwa niaba ya Serikali na kampuni ya Softnet Teknology Ltd pamoja na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). 
 Katibu Mkuu Yambesi alisema kuwa mradi huo unalenga kuweka mtandao mmoja wa mawasiliano Serikalini na taasisi zake na unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU). 
 “Mradi huu ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Serikali Mtandao ukiwa na lengo la kuipatia Serikali na taasisi zake mawasiliano ya sauti, data, nyaraka na picha yenye uhakika, rahisi, salama na yanayopatikana kwa muda wote” alisema Katibu Mkuu Yambesi. 
 Akifafanua kuhusu malengo ya mradi huo Yambesi amesema yanaenda sanjari na malengo ya kujengwa kwa mkongo wa Taifa na utekelezaji wa sera ya Serikali mtandao, Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003, programu ya mabadiliko ya utekelezaji wa kazi na utoaji wa huduma katika katika Utumishi wa Umma. 
 Malengo mengine ni Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA), Mpango Taifa wa Maendeleo ya miaka mitano 2012 hadi 2016 na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...