Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim  akimpokea Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Mhe. Dr. Alberto Antonio Vaquina mara baada ya kuwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Waziri Mkuu huyo ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Eduardo Coloma ni miongoni mwa viongozi wengi kutoka duaniani kote watakaoshiriki Maadhimisho ya kilele cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika tarehe 26 Aprili, 2014.
Mhe. Vaquina akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri Mambo ya Nje Dkt. Maalim wakitizama burudani ya ngoma iliokuwa ikitolewa Viwanjani hapo.
Mhe. Dkt. Maalim akizungumza na Dkt. Alberto Antonio Vaquina, Waziri Mkuu wa Msumbiji mara baada ya mgeni huyo kuwasili.
                                        Picha na Reginald Philip.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...