Ankal Salam Aleikum,

Naomba uniwekee taarifa hii ya zengwe alilokutana nalo dereva wetu wa bodaboda ambaye alikamatwa jana maeneo ya posta na Jamaa wanaojiita TAMBAZA AUCTION MART & GENERAL BROKER sasa baada ya kugoma kulipa fain ya TSH 50,000 jamaa ambaye ndo mkuu wa hicho kikosi kilichokua pale kwenye traffik lights za Serena akasema anatupa kibali cha 20,000....na hata mtoza faini ..sasa angalia angalia hiyo fomu ya faini ambayo jamaa alikua kamjazia ili alipe faini ya 50,000 ...na kesho kaahidi kutoa hicho kibali cha temporary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ni miradi ya watu, sisi wa chini ndio tunao umia.

    ReplyDelete
  2. Jamani hii hali mpaka lini?mii mwenyewe ni mwathirika sana walitoza laki mbili faine eti laki moja Tanroads na laki ingine eti inaingia mfukoni mwa kampuni yao!na nilipaki tu kwa ajili ya kusikiliza tu simu nilipigiwa na mama alikuwa ni mgonjwa na naahidi nikipata muda nitairusha kwa Michuzi na wakati napokea hata sijaongea walitokea na Noah yao nyeupe maendeo ya Mbagala.
    Kwa kweli hizi kampuni ziangaliwe sana tena sana!zinawaumiza wanyonge sana!nami nikiiumbuka pesa yangu na ipo siku wataalaanika tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...