Askofu Sixbert Paul wa kanisa la Victorious la mjini Moshi akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na hafla ya kutunukiwa shahada la udaktari ya huduma
Askofu Sixbert Paul wa kanisa la Victorious la mjini Moshi akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na hafla ya kutunukiwa shahada la udaktari ya huduma


Na Mwandishi wetu, Moshi
CHUO kikuu cha Africa, African Graduate University, Chenye makao yake nchini, Sierra Leone kinatarajia kumtunuku shahada ya udaktari ya huduma, Askofu Mkuu Sixbert Paul, wa kanisa la Victorious, lenye makao yake makuu mjini Moshi, mkoani Kilimajaro, katika hafla itakayofanyika Jumapili hii.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Askofu Sixbert alisema atakabidhiwa shahada hiyo jumapili ya May 18 mwaka huu katika kanisa la Victorious lililopo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Askofu Sixbert alisema pamoja na yeye kutunukiwa shahada hiyo, pia mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Mhando,atatunukiwa cheti maalumu cha kutambua mchango wake wa kueneza injili kupitia uimbaji.


Alisema katika hafla hiyo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Meya wa Mji wa Mshi Bw. Jafary Michael, na kwamba viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika Kusini, Zambia,Uganda , Kenya  na Kongo watahudhuria, akiwemo mpatanishi wa masuala ya kijeshi  anayefanya kazi na umoja wa mataifa Brigedia Timoth Kazembe ambaye anatoka nchini Zambia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...