Moja ya mabasi yanayotoa huduma ya usafirishaji wa abiria ndani ya jiji la Dar es salaam (UDA),lenye nambari za Usajili T 485 CVP na lenye nambari ya idadi 168.usiku huu limepiga mweleka katika eneo la Tabata Shule,mbele ya Hoteli ya Green Light na ubavuni kabisa mwa kituo cha Polisi Tabata.Kamera ya Glogu ya Jamii ilifika eneo hilo na kukuta baadhi ya wahusika waliokuwa wakilitumia basi hilo wakihangaika kutoa baadhi ya mali zao zilizokuwemo ndani ya basi hilo ili waweze kuondoka nazo kwa ajili ya usalama wa mali hizo.Ripota wetu aliposogea na kuwauliza nini chanzo mpaka basi hilo limepiga mweleka huo,hakuna alietaka kujibu swali hilo huku wengine wakijaribu kuipa mgongo kamera yetu.ripota wetu hakuchoka,akajaribu kuwauliza baadhi ya mashuhuda waliokuwepo jirani na eneo la tukio hilo ambao walionekana kulalamika sana huku wengine wakitupia lawama Dereva wa basi hilo kwa kusema "Huu ni uzembe wa Dereva,maana ametaka kusimama gari katika sehemu isiyokuwa na kituo kwa kuchukua abiria mmoja na matokeo yake amesababisha hasara kwa kampuni yake".hivyo ndivyo walivyokuwa wakisika mashuhuda hao.Hadi Tunaondoka eneo la tukio hakukuwa na juhudi zozote za kuliinua basi hilo na wame wahusika waliokuwepo waliondoka.
 Basi hilo likiwa limepiga ubavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2014

    UDA ile ya Mwaka 1978 siki zile sio UDA ya sasa!

    Madereva wake wengi ni Masela tu, bangi nyingi hivyo inabidi kabla ya kutoa kazi tusiangalie Leseni pekee tuwapime na akili na kiwango cha matumizi ya ulevi!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2014

    Mdau wa kwanza kwa nini unamlaumu dereva.

    Hata kama dereva atapimwa akili leo una hakika gani kuwa kesho akili haitayumba tena.

    Hapa dawa ni wajenzi wa barabara kuweka vizuizi ambavyo vitazuia ajali kama hii....

    Je tunahitaji mitaro ambayo iko wazi? na je kama mitaro iko wazi..kwa nini tusiweka uzio ambao utazuia magari yasiingii kwenye mitaro.

    Tatizo ni TANROADS na wizara ya miundombinu wala siyo dereva......

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2014

    Mdau wa pili unaonekana wewe ni afisa wa UDA na unalinda maslahi! Watanzania msitetee vitu ambavyo vinaonekana ni vibovu, hawa jamaa ni ovyo sana fanyeni ukaguzi wenyewe na mtajua hakuna madereva UDA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...