Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yunliang (kushoto), akishuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Hospitali ya Abdulla Mzee Pemba kati ya Naibu Meneja wa kampuni ya JiangSu Provincial Construction Group Co. Ltd Dai Houxiang na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Saleh Jidawi. Hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Naibu Meneja wa kampuni ya JiangSu Provincial Construction Group Co. Ltd Dai Houxiang akielezea mikakati ya ujenzi huo utakaoanza mwishoni mwa mwezi ujao ambao unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 25. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi. Ujenzi huo utagharimu Dola za Kimarekani milioni 13.
Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yunliang (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya waliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Hospitali ya Abdulla Mzee Pemba utakaoanza mwezi ujao. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...