Chuo bora cha Elite Learning cha Mtoni Kijichi kimeahidi kusaidia timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) ili ziweze kusonga mbele katika shughuli zake.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Elite learning institute Co. Hassan Kashoba baada ya kuvutiwa na jinsi waandishi wa habari wanavyojishughulisha kwa vitendo katika shughuli zao za kila siku.
Kashoba alisema kuwa wao mbali ya kusaidia vifaa vya michezo, pia wametoa ofa kwa waandishi wa habari wa Taswa SC kupata mafunzo ya Information and Communication Technology (Tehama), hotel, ualimu wa shule za awali na kompyuta.
Alisema kuwa wanajua kuwa waandishi wana taaluma ambayo wanaifanyia kazi, lakini katika maisha ya sasa, lazima uwe na elimu ya ziada ambayo itakuwezesha kufanya kazi nyingine mbali ya uandishi wa habari.
“Hii ni fursa kwa waandishi wa habari wa Taswa SC, tumeona jinsi gani walivyo mstari wa mbele katika michezo, tena kwa kufanya kwa vitendo, sisi kwa vile tumebobea katika elimu, tumewapa ofa hiyo, ni jukumu lao kuikubali au kuikataa,” alisema Kashoba.
Aliongeza kuwa kwa muda wa miaka mitatu sasa, wameweza kutoa elimu bora kwa wanafunzi wengi wao wamepata ajira na kuamua kupanua wigo kwa waandishi.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary alikishukuru chuo hicho kwa malengo hayo na kuwaomba watimize ili wachezaji wake waweze kutumia vifaa hivyo kwa michezo na kusomea fani nyingine pia.
Mkurugenzi Mkuu wa Elite learning institute Co, Hassan Kashoba (Kushoto) akizungumzia udhamini wake kwa Taswa FC na Taswa queens. Kulia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...