Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha-Rose Migiro akiwasilisha taarifa ya makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala jana (Jumamosi, Mei 3, 2014). Kulia kwake ni Naibu wake Angellah Kairuki na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wiliam Ngeleja.
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia mkutano huo.
Picha na Wizara ya Katiba na Sheria.
Na Omega Ngole
Serikali imesisitiza nia yake ya kuendesha shughuli zake kwa uwazi na kusema maandalizi ya kutunga sheria ya haki ya kupata taarifa kutoka kwa taasisi za umma yameanza kuongeza uwazi katika uendeshaji wa shughuli za serikali.
Akiwasilisha taarifa ya makadirio ya matumizi kwa mwaka ujao wa fedha kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Mei 3, 2014), Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro alisema dhamira hiyo inatokana na matakwa ya Katiba kuhusu haki ya kupata taarifa, Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) na ahadi ya Rais Kikwete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...