Pichani Kulia ni  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimpokea mgeni wake,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya siku 10,ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.


 Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni.

 Ndugu Kinana akisalimiana na Viongozi wa chama serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni,Wilayani Igunga mkoani Tabora,kulia ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama ngoma ya kiasili iliondaliwa wilayani Igunga wakati wa mapokezi ya Ndugu Kinana, ambaye ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa chama hicho,mara baada ku kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani hummo jioni ya leo.
 Ndugu Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard tayari kwa kuvalishwa skafu na kukaribishwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo Wilayani Igunga mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2014

    Katibu Mkuu unaona barabara hiyo imeshaanza kumomonyoka kidogo kidogo na mwishowe itakatika, Je! ktk ziara yako miundo-mbinu itakaguliwa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2014

    Hii ngoma ya kienyeji ya vijana mbona kama miziki ya kisasa?. Au utamaduni ndiyo umebadilika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2014

    hiyo ngoma nliiona wakicheza ktk runinga,lazma uvae miwani ya kuzuwia vumbi.manake utadhani kimepita kimbunga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...