Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wakazi wa Mji wa Tabora Mjini  wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM leo jioni,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amehitimisha siku za ziara yake ya siku 11 mkoani humo,ya  ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana na msafara wake kwesho wataelekea mkoani Singida kwa ziara siku kadhaaa tena.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwafananisha Wapinzani na Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa maneno,hali ambayo imeeleza kuwa kinaweza kusababisha vurugu nchini.
 Kinana akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage ukiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabora leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiapata mlo wa mchana kwa Mama ntilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini ,Mh Aden Rage,katikati ni  Mbunge wa viti maalum CCM mkoani Tabora,Mh.Munde Tambwe wakishiriki pamoja na naye katika mlo huo sambamba na vijana wa mjini Tabora.
 Baadhi ya Wabunge mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo wa Hadhara uliofanyika mjini Tabora,ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya siku 11 ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2014

    Safi saana. Mmmetoka kweli, hongereni sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2014

    Sihasa balaa. 2015 is approaching

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2014

    Hivi wakuu wa mikoa lazima wawe wana CCM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...