Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui ambapo aliwaambia wananchi hao Kilimo cha Tumbaku kiondoe umasikini na si kuongeza umasikini kwa mkulima.
====== ====== =====
Wakulima wa Tumbaku kata ya Ufuluma wamelalamikia kulazimishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ,hata kama sio wanachama,na pia kutolipwa fedha zao kwa wakati.Kinana amewataka wakulima hao kutokukubali kusumbuliwa kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ambavyo baadhi yake vimejaa walaghai na wanyonyaji wa wakulima hao.
Amesema kuwa Wakulima wa zao hilo la tumbaku wamekuwa wakifanya kazi kubwa na ngumu,lakini hawafaidika na jasho la kazi yao,kutokana na kuanzishwa kwa vyama vingi vya ushirika ambavyo vipo kwa faida ya wajanja wachache,hivyo wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa vyama vya ushirika.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa aliongeza kuwa mnamo mwaka 2012 wakulima wa Tumbaku waliibiwa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 16,kama vile haitoshi mnamo mwaka 2013 wakulima hao waliibiwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 12 na umoja wa vyama vya ushirika,akabainisha kuwa kufuatia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha kwa wakulima,mwaka huu tumbaku haitatolewa kienyeji kwa vyama hivyo mpaka wahakikishiwe fedha zao zitalipwaje.
Akabainisha kuwa imefika wakati wakulima wa Tumbaku wajitegemee,wawe huru na kuamua ni wapi wauze tumbaku yao na kwa bei waitakayo ni si kupangiwa na vyama vya ushirika,akaongeza kwa kusema kuwa Wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa Vyama vya ushirika.
Kinana amemaliza ziara yake wilayani Uyui leo na kesho ataunguruma wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Wakazi wa Ufuluma wakishangilia na wengine wakifuatilia jambo kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kata hiyo ya Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora.
Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Ndugu Shaffin Mamlo Sumar akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma mapema leo jioni katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Ufuluma,Wilayani Uyui mkoani Tabora.
Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao jioni ya leo mkoani Tabora
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali mkoani Tabora jioni ya leo,ambapo Walimu waliwasilisha changamoto zao mbalimbali,na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyajibu papo kwa papo na mengine aliahidi kuyafanyia kazi na mengine aliyapatia majibu mapema iwezekanavyo.
PICHA NA MICHUZIJR-UYUI TABORA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...