Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt Rehema Nchimbi jana aliongoza mamia ya wafanyakazi wa Mkoa wake katika kusheherekea siku ya wafanyakazi Duniani inayoadhimisha kila ifikapo tarehe 1 Mei. Wafanyakazi hao kutoka Serikali kuu,Taasisi mbalimbali za Umma ,Serikali za mitaa Pamoja na sekta binafsi wamejitokeza kwa wingi na kusheherekea sikukuu ya wafanyakazi Duniani ambayo imesheherekewa kimkoa katika uwanja wa Jamhuri Mkoa wa Dodoma.
Wakiongozwa na viongozi wao wa vyama vya wafanyakazi walioalanza kwa mandamano kutoka zilipo Ofisi za Bunge hadi uwanja wa Jamhuri na kupokelewa na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto) akiwaongoza wafanykazi wa Mkoa wake kuimba wimbo wa mshikamano wakiwa wameshikana mikono.Mara baada ya kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Mkoa wake katika uwanja wa Jamhuri.
Wafanyakazi wakishangilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi adauniani katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimi akiwahutubia wafanyakazi wa Mkoa wake katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambayo Kimkoa imefanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma
Mkuu wa Mkoa Dkt Rehema Nchimbi aliyekaa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa jumla wa Mei Mos Kimkoa ambao ni chama cha Wafanyakazi wa serikali kuu na Afya TUGHE. Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati Dodoma.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...