Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, asalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo linatarajia kumalizika kesho.

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa leo Mei 9, 2014, linatarajia kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi Kongamano hilo, leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...