Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Dubai, akiwa na mazungumzo na Ndugu Nehemiah Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa NHC , alipomtembelea Ofisini kwake Dubai.

Mazungumzo yao yalihusu maandalizi ya kongamano la uwekezaji katika sekta ya nyumba litakalofanyika Jumeirah Madnat Hotel, Dubai. Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).

Makampuni makubwa ya sekta ya nyumba hapa Dubai pamoja na mengine kutoka Nchi za Muungano wa Ukanda wa Mashariki ya Kati (GCC and the Midle East) yatashiriki. Makumpuni hayo ni pamoja na Nakheel ambalo ndio limejenga The Palm City ya Dubai, Emaar ambalo ndio wamiliki wa Dubai Mall. Mengine yanatoka Qatar, Bahrain, Oman na Saudi Arabia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2014

    jamani naomba ushauri wa kidiplomasia. unawekaje picha ya nyumbani kwako katikati ya bendera ya/za nchi. kwa upeo wangu hii haijakaa vizuri. nashauri katikati ya bendera ingewekwa picha za wakuu wa nchi husika. THIS IS A SHAME.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2014

    Mhe Balozi nyuma ya bendera ya nchi kwenye Afsi za Serikali weka picha za Wakuu wa Nchi sio ya familia yako. Diplomasia yenu ya siku hizi ikoje??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...