Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiwasalimia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Katume,Mama Fatma Karume akiongea kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka Wazanzibar kuacha kabisa kuuchezea Muungano kwa kuwafata watu wanaoupotosha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akimpongeza Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Katume,Mama Fatma Karume mara baada ya kuzungumza na wazanzibar jioni ya leo waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Demokrasia ,Kibada Maiti mjini Unguja.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwaeleza wananchi wa Unguja kuhusu umoja ulioanzishwa wa baadhi ya vyama siasa na malengo ya umoja huo,wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar. 
Mbunge wa Viti Maalum CCM,Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubiwa wananchi wa Zanzibar kupitia Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar jioni ya leo.ambapo amewataka Wazanzibari kutohadaishwa na UKAWA kususu swala la muundo wa Serikali katika mchakato wa Katiba.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini,Mh. Emmanuel Nchimbi akinukuu sehemu ya maandishi yaliopo kwenye kitabu cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    hivi kwanini tunang'ang'ania hili dubwana muungano? hamuoni jinsi tunavyofarakana, kisa muungano?!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2014

    Mdau wa kwanza Muungano ni Muhimu sana ktk Tanzania!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2014

    Sheikh Abdulrahman Kinana mpe vodonge vyake Maalim!.

    Kofia umekutoa sana pia muulize Shikh Seif Maalim mbona yeye siku hizi ananyoa nywele ktk mtindo wa Pank na amenyoa ndevu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2014

    siasa bwana,ummi mwalim naona kavaa kilemba,kinana kaanguka na kofia ya kiua,si kawaida yao.inabidi uwe kama wao ili uwateke.safi sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2014

    Ni hatari sana wa Mdau 3 kama unavyo sema ukikuta mtu ni mzee akiitwa MAALIM ana nywele nyeupe NA NDEVU ZAKE NYINGI TU lakini ghafla anaacha kuvaa kanzu, ananyoa nywele ktk mtindo wa Punk na ananyoa ndevu!

    Kweli Sheikh wa namna hiyo anaaminika?

    Sheikh huyo kweli atakuwa na busara na akili sawa na umri alio nao?

    Je, Maalim anayenyoa Panki na kunyoa ndevu unaweza kumuamini kama atashika simu yako yenye Laini mbili?

    Ni kuwa akiishika simu yako hatakuwa mstaarabu kutumia Laini moja inayotoka tu, NI LAZIMA ATATUMIA LAINI YA PILI ISIYOTOKA maana ni Maalim asiye aminika!

    La hasha sio rahisi ni kuwa Sheikh huyo kama tunavyoona kauli zake ni za kichochezi akiwa na nia ya kuvunja Muungano !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...