Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii Dkt.Seif Rashid (MB) amehutubia katika mkutano wa 67 wa shirika la Afya Duniani, katika hotuba yake alieleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Tanzania katika sekta ya Afya.Baadhi ya mambo aliyoyaeleza ni Pamoja na mafanikio ya utekelezaji wa Malengo ya millennia hususani lengo la milenia namba nne linalohusu upunguzaji wa vifo vya watoto.vile Vile alieleza mafanikio yaliyofikiwa katika kapunguza maambukizi ya virus Vya ukimwi kutoka asilimia 5.7 mwaka 2007 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012 yote haya yamewezekana kwa sababu ya uwekezaji mkubwa katika maeneo haya Pamoja na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt. Jakaya Kikwete katika kukabiliana na adui Maradhi.
Mawaziri wa Afya wa Tanzania dr.seif Rashid (Mb) na mh. Juma Duni Haji (Mb), waliokaa nyumba Yao ni Mganga mkuu wa serikali dr. Donnan Mmbando Pamoja na dr.Catherine Sanga mwabata wa wizara ya Afya na ustawi wa Jamii katika ubalozi Tanzania nchini Geneva wakisikiliza mada mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...