MBUNIFU na mwanamitindo (model) Rodrick Charles
maarufu kwa jina la ‘Rodney de lativo’ amefariki dunia jana (Mei 30) baada ya
kuugua kwa muda alipokuwa amelazwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo.
Akizungumza na Mtandao huu mapema leo kwa
njia ya simu, Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu, David Msangi
alisema marehemu alipatwa na umauti alipokuwa akiendelea na matibabu katika
Hospitali ya Lugalo, alipokuwa amelazwa na msiba huo hupo nyumbani kwa marehemu
Tabata Bonyokwa, Dar.
“Tumempoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na
mawazo mengi ya kufikia mafanikio yake. Tutaendelea kumkumbuka.” Alisema
Msangi ambaye pia alikuwa mshahuri wa karibu wa marehemu", Msangi alisema.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu,
anatarajiwa kuzikwa hiyo Jumamosi Mei 31huko huko kwenye makaburi ya
Tabata Segerea.
Wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye
majukwaa mbalimbali na wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally
Remtullah, Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin
Kadinda, Justine, Faustine Simon na wengine wengi.
Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshahuri
na model wa kampuni ya Crisswelly African Fashion.
Mareehemu alizaliwa Mei 26, 1994. Elimu yake
alisomea Magoze Sekondari na kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja
kwenye fani ya uwanamitindo na kuendelea hadi alipokutwa na umauti.
Aidha, kwa jamaa wa karibu na wabunifu na
wanamitindo kwa watakaotaka maelezo ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana
na David Msangi kwa namba hii 0652901684
..Rest In Peace Rodney. I remember you forever.
Rodney enzi za uhai wake
Aidha kwa taarifa zaidi:
TAARIFA ZA FAMILIA NI KWAMBA MSIBA UPO BONYOKWA JIJINI DAR ES SALAAM. PANDA GARI YA TABATA SEGEREA SHUKA MWISHO WA GARI KISHA PANDA GARI ZA BONYOKWA SHUKA MWISHO NDIPO MSIBA ULIPO WA NDUGU YETU MPENDWA RODNEY TUTA MUHIFADHI KESHO SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 ALASIRI
UKIWA NI MMOJA WAPO WA MDAU WA TANZANIA FASHION NA Crisswelly African International Fashion, MODEL AU DESIGNER NIVEMA KUJITIKEZA NA KUSHIRIKI KUMSINDIKIZA SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU RODNEY.
PIA WAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA MAMA Asya Khamsin KWA TIGOPESA NO0713263363
MUNGU AKUBARIKI TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU KWA MARAFIKI ZAKO UTABARIKIWA AMEN!!!!!!!!!!!!!!
KWA MAELEZO WASILIANA NA #CRISSWELLY NO 0714802527
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...