Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Aprili umeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Aprili 2014 umeongezeka na kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 za mwezi uliopita.
Amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Aprili 2014 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Machi huku kukiwa na ongezeko dogo la upandaji wa bei kwenye baadhi ya bidhaa na huduma kwa mwezi huu ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...