Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni inayojumuisha wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Pwani (Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo) na mkoa wa Tanga Bi Zahra Kayugwa akimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda alipotembelea katika banda la PPF, pembeni yake ni Makamu wa Rais Viwanda – TCCIA Makao makuu ,Ndugu Yakub Hasham. Mfuko wa PPF unaandikisha wanachama kutoka katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
Afisa Mwandamizi wa PPF Kanda ya Kinondoni Bi Upendo Mazzuki akitoa elimu kwa mwanachama aliyetembelea banda la PPF wakati wa Maonesho ya 2 ya Kibiashara mkoani Tanga.
Afisa Mwandamizi Uwekezaji wa PPF Bi Anna Shayo akitoa elimu kwa mwanachama aliyetembelea banda la PPF katika viwanja vya Tangamano.
Maafisa wa PPF Kanda ya Kinondoni Ndugu Jabir Bundile (wakwanza kulia) akifuatiwa na Ndugu John Nyalusi wakifuatilia maelezo ya mwanachama aliyetembelea katika banda la PPF.
Afisa Mhandisi wa Mifumo ya Habari ya PPF Bi. Isabella Ngalawa akitoa elimu kwa mwanachama aliyetembelea banda la PPF wakati wa Maonesho ya 2 ya Kibiashara mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano .
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni inayojumuisha wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Pwani (Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo) na mkoa wa Tanga Bi Zahra Kayugwa na Afisa Masoko wa PPF Bi Nelusigwe Mwalugaja wakifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Ndugu Absalom Kibanda akijisajili katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF lililopo viwanja vya Tangamano, mjini Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...