Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda
kuwataarifu wananchi wote kuwa, hivi karibuni kumekuwa na watu au kikundi cha watu
wanaosambaza taarifa potofu kwa wanachama wa PSPF kwa njia ya ujumbe mfupi wa
simu ya mkononi kwa nia ya kuwatapeli.
Taarifa hizo zinazotolewa siyo sahihi na PSPF
inawaomba wanachama wake kuchukua tahadhari dhidi ya ujumbe huo wa kupotosha
unaosambazwa kwa njia ya simu na watu au kikundi cha watu wakidai kuwa ujumbe
huo unatoka PSPF.
PSPF inatoa huduma mbalimbali kwa wanachama wake bila sharti
lolote wala malipo ya namna yoyote. Ujumbe wowote unaomtaka mwanachama kutuma
fedha kwa ajili ya kulipia huduma yoyote inayotolewa na Mfuko siyo sahihi na ujumbe
wa namna hiyo hautolewi na PSPF. Hivyo, ninawaomba wanachama wa PSPF kuwa
makini na ujumbe huo unaosambazwa na watu wachache ambao wanataka kuuchafua
Mfuko na kujinufaisha kwa njia zisizo halali.
Iwapo itatokea mwanachama amepata ujumbe wenye utata,
tafadhali piga simu katika Kituo cha Huduma kwa Wateja wa PSPF kwa kutumia
namba 022 5510400 au fika katika ofisi ya PSPF iliyopo karibu
nawe au toa taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe kwa hatua
stahiki.
Taarifa hii imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF,
Makao
Makuu, Golden Jubilee Towers, S. L. P. 4843, Dar-es-Salaam.
Simu:
+255222120912/52 au +255222127375 /6
Nukushi:
+255222120930
Barua
pepe: pspf@pspf-tz.org
Tovuti:
www.pspf-tz.org
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...