MAZISHI LEO JUMAMOSI TAREHE 17.05.2014 

SHUGHULI ZOTE ZITAFANYIKA NYUMBANI KWA BW. SALVA RWEYEMAMU KINONDONI, MKABALA NA VIJANA HOSTEL NA MANGO GARDEN, JIJINI DAR ES SALAAM

SAA      1.00:  ASUBUHI KIFUNGUA KINYWA - NYUMBANI

SAA 4.00-5.00:  CHAKULA CHA MCHANA - NYUMBANI

SAA 5.00-6.00: KUAGA MWILI - NYUMBANI

SAA 6.00-7.00: MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA

SAA  8.00 Mchana: SHUGHULI ZA MAZISHI MAKABURI YA KINONDONI
---------------------------------------------------------------
WASIFU WA PRIVATE  BRIAN SALVA RWEYEMAMU


Rwechungura Brian Salvatory Rweyemamu, aliyefariki dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.
Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar es Salaam kabla ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.

Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni, Dar Es Salaam, mwaka 1998.

Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999, ambako alikaa miaka minne kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.

Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.

Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.

Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe 10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza fahamu.
Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2014

    r i p kamanda mbele yako nyuma yetu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2014

    Inasikitisha kijana mdogo kweli.
    Poleni wafiwa.
    Mungu amuweke mahala pema peponi. Yaani machozi yananitoka!

    ReplyDelete
  3. BridgetyMay 16, 2014

    Lala salama mpz wangu., will always love u. R.I.P my love. Bridgety

    ReplyDelete
  4. Can not believe you are gone so young... I met you when you were in Brussels, good, confident, fun and full of humour. I remember you loved elvis Presley , so sad that it's this dreaded disease that's taken you, rest in pease Brian. My sincere sympathies to all your family. Poleni sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2014

    Very sad!

    Ameondoka akiwa mbichi, pia tumeona na kujifunza jinsi Mzee wake alivyo mweka kwa kumpa msingi mwema wa maisha kwa kumpeleka Jeshi JKT badala ya kumpa kazi ya Ofisini licha ya nafasi kubwa Serikalini aliyo nayo.

    Poleni sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2014

    RIP. Gone too soon

    ReplyDelete
  7. R.I.P. Brian inasikitisha sana umeaga dunia ukiwa bado mdogo mno. poleni sana wafiwa. hakika inaonyesha jinsi wazazi wake walivyompenda na kumuendeleza kielimu kiasi hicho. lakini mungu amempenda zaidi. sisi wote tunakufuatia katika njia hiyo hiyo. By Deogratias Michael.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...