MAREHEMU MOSHI CHANG’A 
Bismillah Rahmani Rahim
Familia ya akina MWACHANG’A wa Iringa inatoa shukurani za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioshiriki kwahali na mali kuanzia kumuuguza mpaka kufanikisha mazishi ya mpendwa wao marehemu MOSHI CHANG’A aliyefariki siku ya Jumapili tarehe 20.04.2014 katika hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Kihesa mkoani Iringa Mjini katika makaburi ya Mtwivira, siku ya Jumatano tarehe 23.04.2014.
Aidha shukurani za pekee zimuendee Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa faraja kubwa aliyoitoa toka kumuuuguza marehemu mpaka alipofariki na kuzikwa.
Shukurani za dhati zimuendee Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda (Mb) kwa nasaha zenye faraja kubwa alizozitoa katika kipindi chote kuanzia kuuguza na  nasaha alizozitoa wakati wakuaga mwili wa marehemu pale Mbagala.
Shukurani nyingi kwa Mh. Waziri Hawa Ghasia, mawaziri na makatibu wakuu wote walioshiriki na kutufariji katika msiba huu.
Tunawashukuru mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Mh. Said Meck Sadick, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na mwenyeji wa mazishi Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Tunawashukuru zaidi Viongozi wote wa serikali wakiwemo Mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Madiwani wa wilaya zote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi chote cha kuuguza mpaka mazishi ya marehemu.
Aidha shukurani za pekee zimuendee Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda kwa faraja kubwa aliyoitoa kwa wafiwa hasa siku ya mazishi pale Iringa mjini, Mbunge wa Iringa Mjini na wabunge wote waliotufariji kwahali na mali ahsanteni sana
Mstahiki Meya wa mji wa Iringa Mh. Mwamwindi, viongozi wote wa vyama vya siasa na serikali wangazi zote mkoani Iringa, Mashehe walioongoza na kusimamia mazishi na viongozi wadini mbalimbali walioshirikiana nasi kwenye msiba huu tunawashukuruni sana.
Aidha shukurani za pekee ziwaendee Madaktari na wauguzi wote wa hospitali ya Muhimbili kwa tiba nzuri na juhudi kubwa walizofanya ili kuokoa maisha ya marehemu katika kipindi chote cha kuugua kwa marehemu nasema ahsanteni sana
Hakika sirahisi kumtaja kwajina kila mmoja wenu, aliyetufariji na kutusaidia kuanzia kipindi cha ugonjwa, mazishi mpaka baada yamazishi, lakini fadhila zenu kamwe hazitosahaulika,  na kwamba shukurani zetu zimfikie kila mmoja wenu na kwamba tunamuomba Allah Subhana Wataalah awalipe yaliyo mema hapa duniani na kesho akhera In Shaa Allah.
Mwisho tunaishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa misaada, faraja na ushirikiano mkubwa iliotupatia katika kipindi chote cha tiba, mazishi na mpaka baada ya mazishi.
INA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAJIUN

                                        Familia ya Wafiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...