Mjumbe kutoka Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na wabunge wengine kutoka nchi washiriki wakifuatilia mada kwa makini
   Katibu Mkuu wa CPA Dkt. William shijja akifafanua jambo wakati Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Bunge la Ghana ambaye pia ni Waziri anayeshughulikiwa maswala ya Bunge Dkt. Benjamini Bewa- Nyang Kunbour akiwasilisha mada yake kuhusu Mahusiano  ya Mbunge na chama chake wakati wa siku ya pili ya semina ya 25 ya Chama cha Mabunge wanachama wa jumuiya ya Madola CPA
 Mbunge kutoka News Zealand Asenati Lole- Taylor akichangia uzoefu wan chi yake baada ya kuwasilishwa mada kuhusu Mahusiano  ya Mbunge na chama chake na Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Bunge la Ghana Dkt. Benjamini Bewa- Nyang Kunbour.
--------------------------
Wabunge kutoka nchi kadhaa barani Afrika na nje ya bara hilo wamelalamikia uelewa mdogo miongoni mwa wananchi wa kawaida kuhusiana na majukumu ya wabunge na kuwafanya wananchi hao wawaone wabunge wao kama chanzo kikubwa cha fedha. 
 Malalamiko hayo yalitolewa jana na wabunge kadhaa wanahudhuria semina ya 25 ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola, inayofanyika jijini Dar es Salaam. Mjadala kuhusu suala hilo uliibuliwa na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Prof David Mwakyusa (CCM), wakati akichangia mada kwenye semina hiyo. 
 Mbunge huyo ambaye ni mongoni mwa wabunge kadhaa wanaoliwakilisha Bunge la Tanzania kwenye semina hiyo, alisema kuwa wananchi wengi hawaelewi maana hasa na wajibu wa mwakilishi wao kwenye chombo cha kutunga sheria.
 “Watu wengi wanamuona Mbunge kama mtu mwenye fedha nyingi sana ambaye anapaswa kuwatatulia matatizo yao mbalimbali kama vile kulipa ada kwa ajili ya mtoto, kulipia gharama za matibabu au kumalizia ujenzi wa nyumba,” alisema na kuongeza:
 “Matokeo yake, kila Mbunge unapoonekana kwenye jimbo lako wananchi wanaona kama Benki ya Dunia ndogo imekuja na hivyo wanajipanga wakisubiri kupata chochote kutoka kwako.” 
 Ingawa Prof Mwakyusa alitoa hoja hiyo akidhani kuwa ni tatizo hilo linawakabili wabunge wa Tanzania tu, wakati wa mjadala huo ilibainika kuwa tatizo hilo limeenea barani Afrika na nje ya bara hilo, hasa katika nchi zinazoendelea. 
 Mwasilishaji wa mada iliyozua mjadala huo, Dk Benjamin Bewa-Nyong Kunbour, ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Bunge la Ghana na Waziri wa Masuala la Bunge, alibainisha kuwa tatizo hilo lipo pia nchini kwao. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2014

    Lazima wananchi wawaone ni ATM maana mkishinda ubunge, Waheshimiwa hupongezwa kwa sababu ''wameula'' na siyo kwanza kutatua shida za wananchi kwa wabunge kuibana serikali ielekeze fedha kwa huduma za bure za afya na elimu.

    Mtawaambia wananchi kuwa wabunge si ATM huku mnapata posho nono, magari ya kifahari ya ubunge, hamtumii usafiri wa umma kama treni au mabasi.

    Pia mnaacha kazi zenu za taaluma kama uprofesa, udaktari n.k na wote mnakimbilia 'ulaji' bungeni lazima wananchi wajue vipi nyote mnakimbilia nyadhifa za kisiasa lazima kuna ulaji mkubwa sana.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2014

    Mbona wakati wa kampeni mnawapa? Hizo bodaboda, bajaji, vifaa vya ujenzi, fedha taslimu mnazigawa za nini sasa hivi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...