Na Abdulaziz Video, Ruangwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa walemavu watatu katika
shughuli fupi iliyofanyika katika Kata ya Mandawa wilayani Ruangwa
mkoani Lindi
Shughuli ya makabidhiano inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais
aliitoa kwa walemavu hao watatu ili kufuatia ahadi aliyooitoa Mwishoni
mwa mwaka jana alipokutana nao alipokuwa katika ziara yake mkoani humo
kukagua shughuli za maendeleo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Niaba ya Rais
Kikwete Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo
hilo Kassim Majaliwa amewaambia walemavu hao kuwa Rais Kikwete
amefurahi sana kutimiza ahadi hiyo ili kusaidia kuchangia uchumi wa
walemavu hao ili wajiongezee kipato chao
Aidha Majaliwa aliwaagiza Viongozi wa kata na kijiji kutoa usaidizi wa
kutunza na kusimamia matumizi ya bajaji hiyo ili Iweze kuwa salama na
walemavu hao kunufaika na msaada wa Rais
Kwa Upande Katibu Tawala wilaya ya Ruangwa ,Silvanus Kilowoko alieleza
kuhusiana na Msaada huo alieleza kuwa ofisi yake ilipokea fedha za
kununulia bajaj hiyo na tayari wamefanikisha kuisajiri kabla ya
kukabidhiwa kwa walengwa
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Ya walemavu hao ambao ni Saidi
Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan , Mwenyekiti wa CCM
Wilayani humo Bw Issa Njinjo kwa upande wake alisisitiza juu ya
matumizi ya bajaj hiyo ikiwemo kujiongezea kipato
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akikabidhi Bajaji hizo kwa walengwa
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akimkabidhi Bi Nassim Ramadhan Bajaji yake
Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo
walemavu waliokabidhiwa Bajaji Saidi Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan wakifurahia zawadi hizo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...