Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wa kwanza kulia na ujumbe wake akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki hayupo pichani jijini Istambul siku ya Ijumaa tarehe 09 Mei, 2014. Mhe. Membe aliliomba Shirika hilo liingie ubia na Shirika la Ndege la Tanzania. Ombi ambalo Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kulifanyia kazi ambapo wiki ijayo atatuma timu ya wataalamu ili kuongea na timu ya wataalamu ya ATCL kutathmini namna mashiraka hayo yatakavyoweza kushirikiana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki wa katikati pamoja na timu yake ikimsikiliza kwa makini Waziri Membe hayupo pichani.
Ujumbe wa Tanzania na wa Shirika la Ndege la Uturuki wakiendelea na mazungumzo
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki akifanya power point presentation kuhusu utendaji wa shirika lake na matarajio ya kibiashara katika Bara la Afrika na ulimwengu wote kwa ujumla. Alitaja Bara la Afrika kuwa ni bora zaidi kibiashara katika siku zijazo kutokana na ukuaji wa uchumi wa kasi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki
Waziri Membe kushoto naye anapokea zawadi yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki
zawadi kwa Waziri Membe.
Mkutano wa Waziri Membe na Wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kati) akiwaeleza wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki (baadhi yao wanaonekana katika picha ya chini) fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania. Aliwahamasisha waje kuwekeza Tanzania hususan, katika sekta zitakazoongeza ajira kwa wingi kama vile viwanda vya nguo na kilimo. Wafanyabiashara hao walionesha dhamira ya dhati kuja nchini kuangalia fursa walizotangaziwa.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Uturuki na ujumbe wa Tanzania.
Waziri Membe akibadilishana kadi za mawasiliano na Wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2014

    Jamani huo uwanja mpya wa ndege unaojengwa Dar kama utakuwa wa kisasa naomba serikali ijaribu kuongea na Marekani ili tuwe na direct flight toka USA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2014

    Hizo zawadi ni za taifa au ni za membe binafsi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2014

    Hahah mdau hapo juu umechekesha, swala ni biashara, kama kuna wateja ndege zitakuja tu wala hakuna majadiliano. Unatakiwa kujua kwamba mashirika ya ndege Marekani ni biashara binafsi, sio kama ATC. Hata ATC hawapangiwi trips na JK wala mwanasiasa yeyote. Shirika linajiendesha lenyewe.Nilishasikia Continental Airline? walikuwa mbioni kuanzisha direct flight from Texas to Dar, sijui imeishia wapi.

    Mghaibuni

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2014

    hakuna ndege hata moja inayotoka states kuja Africa.wanaishia huko huko.hawataki ubabaishaji.huyu bwana waziri anataka ushirikiano wa aina gani manake ATCL wana kadege kamoja tu.wamekopa hela kununua ndege mpya matokeo yake wameleta ndege chakavu ya 540.Ng'ombe wa masikini kweli hazai,na akizaa.......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...