Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mapema Machi mwaka huu
alikabidhiwa nishani ya kumbukumbu ya Profesa M.O. Oyawoye aliyewahi kuwa
Profesa wa kwanza duniani kutoka Bara la Afrika katika masuala ya jiolojia huko
nchini Nigeria. Profesa Muhongo alikabidhiwa nishani hiyo na timu ya wanajiolojia kwa
kutambua mchango wake mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Nishani hiyo
alikabidhiwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay kwa niaba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa ofisini kwake huku akiwa
amevaa nishani hiyo
Well deserved prof!
ReplyDeleteMghaibuni
Nishani hii na kazi zako ulizowahi kufanya zitakuwa na maana kama hutafanikiwa binafsi katika kazi yako ya sasa kama waziri wa nishati bali litafanikiwa taifa kwa mchango wako katika kuondoa tatizo la umeme na kuchangia watanzania kuhusishwa moja kwa moja kwenye umiliki na uzalishaji wa vitalu vya mafuta na gesi, vinginevyo hilo litabaki kuwa pambo binafsi.
ReplyDeletesesophy
Wanatutafuta hawa wanigeria wameanza na Raisi wetu
ReplyDelete