Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Wakili Damas Ndumbaro akitoa tamko la kumuondoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba SC,Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti,Michael Richard Wambura kwa kosa la kufanya kampeni kinyume na kanuni na sheria za Uchaguzi za TFF.Ndumbaro ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya Kamati yake kukaa na kujadiliana mambo mbali mbali kuhusu Uchaguzi huo Mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29,2014,na kubaini kosa alilolifanya Wambura la kuanza kampeni mara baada ya kurudishwa kwenye kinyang'anyiro hicho.Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Issa Batenga.
 Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Bw. Amin Bakhresa akijibu moja ya mashwali yaliyoulizwa na waandishi wa habari juu ya uamuzi wa Kamati kumuondoa kwenye Uchaguzi Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti,Michael Wambura.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini Mkutano huo,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2014

    Hii kamati ina watu wazima ila mambo yao na maamuzi wanayoyafanya hayaendani kabisa. Ina onyesha wazi wana chuki na maslahi binafsi na ndivyo viinavyotawala maamuzi yao

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2014

    Dhahiri wambura anajua mengi,hawa wanaendekeza chuki zao. Wambura komaa mpaka uzibe mirija yote inayotafuna maendeleo ya soka la tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...