MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI, SAID WA NGAMBA MAARUFU KWA JINA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU YA KIHARUSI. ALIKUWA NA MIAKA 59.

AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL, MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA AMBAPO MAZISHI YANATARAJIWA KUWA KESHO SAA KUMI ALASIRI KATIKA MAKABURI YA  TABARA SEGEREA JIJINI DAR ES SALAAM.

MZEE SMALL ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WACHEKESHAJI MAHILI KUTOKEA HAPA NCHINI, MARA KWA MARA AKIWA NA "MKEWE" WA JUKWAANI BI. CHAU.

MAISHA YA SANAA YA MZEE SMALL YALIANZIA KATIKA NGOMA ZA UTAMADUNI, AKIWA MMOJA WA WASANII WALIOKIWEZESHA KIKUNDI CHA MAGEREZA KUTAMBA SANA TANGIA MIAKA YA 1970 NA 1980. 
ALIENDELEA KUWA NYOTA WA UTAMADUNI HATA BAADAYE ALIPOSTAAFU MAGEREZA NA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA RELI "KIBOKO YAO" NA BAADAYE NASACO,  KABLA YA KUANZISHA KUNDI LAKE MWENYEWE NA HATIMAYE KUJITOSA KWENYE FILAMU, AKIWA MUIGIZAJI WA KWANZA KUCHEZA KOMEDI KWENYE TV.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA INAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
-AMIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2014

    Innalilahi wa innailayhi rajiuun.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2014

    RIP MZEE SMALL

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2014

    Innaa liLlaahi wa innaa ilayHi raajiuwn.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2014

    inna lillah wa inna ilayhi rajiun

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2014

    Sooo sad, huyu bwana alikuwa na kipaji...RIP

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2014

    RIP Mzee Small. Asante kwa kutuburudisha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2014

    R.I.P Mzee wetu

    ReplyDelete
  8. Nakuja haina hatakayedumu milele nasi tupo foleni.
    Pumzika kwa amani MZEE wetu

    ReplyDelete
  9. INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN. Mwenyeez Mungu akughufirie kwa yote, akupumzishe pema unapostahiki na kesho uwe miongoni mwa waja wake wema katika yake Jannatu N'naeem.

    Kwa kweli kila nlipokuwa naiona hii kofia ya 'Tarbush' popote pale, cha kwanza hupata picha ya Mzee Small, gwiji wa vichekesho Tanzanzania. Rest In Peace Marehemu mzee wetu Bw. Said Ngamba almaaruf 'Mzee Small'.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...