Watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha kwenye ajali ya Daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo - Tegeta jijini Dar mchana huu,baada ya kushindwa maarifa ya kiudereva kwa Dereva wa daladala hilo hali iliyompelekea dereva huyo kuhama mpaka upande wa pili wa barabara na kulivaa lori kwa nyuma.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.
Hili ndilo lori lililokuwa likipita katika upande huo wa Barabara na kufatwa na daladala hiyo.
Huyu dereva alikuwa anawahi wapi, amepoteza roho za watu bure, kama atakuwa hajafa basi sheria ichukue mkondo wake. Mungu azilaze mahali pema peponi Amiiinaaa. R I P wote.
ReplyDeleteHicho kipande cha barabara kimewekewa alama za barabarani karibu kila baada ya mita 200.Maximum Speed ni 60Km.Kukiwa na foleni huwezi kugundua kama ni kipande hatari, lakini ni hatari.Speed rader (vitochi) vitumike au matuta yawekwe.Pole kwa familia ziliopotelewa na wapendwa nwaombea majeruhi wapone haraka.
ReplyDeleteDavid V
Innalillahi wa Inna ilayhi rajiun...Poleni wafiwa
ReplyDeletepolen sana ndugu zetu
ReplyDeleteHabari za TV zinasema watu 6 ndio wamekufa na wengine 12 wamejeruhiwa
ReplyDeletejamani day waka watatimaliza!
ReplyDeleteBado speed limit. hawajaweka, madreva kuweni makini jamani
ReplyDeleteHizi ajali zime kuwa too much.Nadhani umefika wakati sheria za barabarani zipitiwe upya na kufanywa kuwa kali zaidi kwa wa kiukaji.Vilex2 jeshi letu la Polisi inabidi libadilike na kuacha kufanya kazi kwa mazoea lazima liende na wakati ili kuweza kukabiliana na wavunja sheria.
ReplyDeletetatizo polisi wako bize na dili za kukakamata bodaboda na bajaji tu ,mambo ya kuangalia sheria za barabarani hayapo katika manifesto yao!!kwa hili hii ajali za kijinga kama hizi hazitapungua!!!
ReplyDeleteMdau mikocheni
Jana ...wizi wa maafuta....juzi roli limevunja daraja...leo haya yanatokea.....bado nafikiria kurudi........R.I.P
ReplyDeleteDaaaaaaaah...mungu azlaze roho za marehmu mahali pemas peponi
ReplyDeleteToo bad ila uzembe wa madereva kamwe abiria pia hawatakiwi kulifumbia macho suala la Ku overspeed.majina ya waliofariki na majeruhi yawekwe ili kusaidia utambuzi.RIP
ReplyDeleteMynz mungu awarehemu marehemu na kuwafanyia wepesi majeruhi,kaka hongera sana Kwa kuwasitiri victims wa Ajali Kwa kutotoa picha zao,mablogger wengine wajifunze kutoka Kwako
ReplyDeleteMadereva wengi wa siku hizi kwa kweli sijui wanajifunzia wapi udereva! wao ndio wamekuwa chanzo no1 kwa ajali za siku hizi. Hawana umakini kabisa. wamegeuza magari yamekuwa kama bodaboda. hawana umakini kabisa wanapoendesha.
ReplyDelete