Wadau tuwe makini wapi unapeleka kuosha gari lako. Vinginevyo utaishia kuoshewa wese lote kama hivyo...
Ankal. Kuna jamaa katoa maoni kuwa hatarudi Bongo baada ya kuona picha kwenye Globu ya Jamii ya mtu kuiba wese kutoka kwenye gari. Ndugu kama huyo ni mmoja ya wanaopenda sana kuiponda nchi yao kama vile pote pengine ulimwenguni ni pepo. Ashakhum si Matusi Ankal, Rusha hii wapondaji wakuu wa nchi yao (wajionee wenyewe hao wanaowaita wastaarabu huku wakidai hawarudi Bongo) wakitia BIOFUEL kwenye tanki la mtu.
Too bad
ReplyDeletehii tabia ya wizi imeota mizizi
something has to be done
Inabidi sasa tuwe makini maana hua wana eka maji
DeleteNafikiria sana kuhusu kurudi nyumbani.....kwakweli wenda nikajikataa mazima hukuhuku....
ReplyDeleteAma kweli kufiri ni mzigo kwa baadhi ya watu.Haiingii akili mtu kukana kwenu kwa kuogopa wizi!mbona hata Ulaya na USA wizi upo?
ReplyDeleteNiko bongo baba/mama. Nachokoza tu
ReplyDeleteAnonymous hapo juu wewe umeshaamua hurudi nyumbani, hapa ni unatafuta tu sababu za kuhalalisha kutokurudi kwako.
ReplyDeleteKuna sehemu rasmi za kusafisha magari, tutumie hizo, kwa kiasi ni salama. Pia funga gari wasafishe nje kwanza, wakisafisha ndani simama hapo uwaangalie, watu si waaminifu.
Mdau wa nne naunga mkono maoni yako. Hao wenye dhana hiyo ya kuogopa kurejea makwao ati kisa kuogopa matatizo au mambo kama hayo yatokeayo kila siku, mbona kote duniani yapo. Sana sana huwa tunatofautiana na mazingira na the way kila watu wanavyopractice maovu hayo, depends on the environments they're living in. Ila kote utapeli, wizi, ulaghai na vijitabia vyote hivyo vipo dunia nzima, hakuna muwaridi wowote ule na popote pale ulokosa kuwa na miba.
ReplyDeletejamaa anashindwa kujielewa kuwa dunia inafanana tofauti ni rangi tu za watu ... lkn matendo yanafanana
ReplyDeleteHiyo inaitwa kupiga nyoka!!
ReplyDeletePoint well said mdau HK.Maovu yako kila mahali na kuna mengine yanatokea huko majuu na hayaja happen hapa nyumbani.ie kuna incidences nyingi za machizi kuingia kwenye Malls,movie theatres etc na kuua watu wasio na hatia kitu ambacho kwa hapa nyumbani so far ni unthinkable even though sio impossible.nini kuibiwa mafuta ya gari!!!
ReplyDeleteDuh
ReplyDeleteNaomba kutofautiana na waliotoa maoni kwa kuzingata hiyo picha hapo.
ReplyDeleteHii picha sidhani kama ina ukweli; japo imefanya watu wachangie.
'Huyo mtu anayeonekana kuweka hiyo BIO-FUEL kwenye gari ya mtu alipataje access wakati release handle ya fuel tank iko ndani? najua magari ya zamani unafunua tu kwa nje; ila mengi ni kwa funguo. Hii fotoshopu imeleta mtiririko wa maoni. Nawakilisha.
Pia kusema hivyo sina maana tabia kama hizo hazipo; nina shaka tu na aliyetuma mada. Alitaka watu watoe maoni