Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Mkoa wa Mbeya Vivianus Rwezaura akikabidhi
kombe kwa nahodha wa timu ya Green City, Issa Nelson baada ya timu hiyo
kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six Kanda ya Kusini.
Mashindano
ya Castle Lager Perfect Six ngazi ya fainali za Kanda yamefikia tamati
kwa kishindo baada ya timu ya Green City ya Jijini Mbeya kufanikiwa
kutwaa ubingwa wa Castle Lager Perfect Six baada ya kuichabanga Timu ya
Savannah kutoka Mkoani Iringa kwa mabao 8-3.
Michuano
hiyo ambayo ilichezwa katika Viwanja vya City Pub, jijini Mbeya ulikuwa
ni wa vuta nikuvute huku kila upande ukitaka kuchukua ubingwa wa kanda
hiyo kuungana na kanda zingine saba Jijini Dar es salaam katika fainali
ambazo zitawapatia washindi fursa ya kwenda kutembelea uwanja wa Camp
Nou kushuhudia mechi za FC Barcelona na kutembelea maeneo mbalimbali ya
jiji la Barcelona. Kanda ya kusini ndio imekamilisha mchakato wa kupata
wawakilishi wa kanda ambazo zitashiriki kwenye fainali za taifa
zitakazochezwa mwezi Agosti jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ulihusisha timu nne kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Timu
zilizoshiriki katika mchuano huo ni Green City na White Stars kutoka
Jijini Mbeya,Savannah na Gaddafi kutoka Manispaa ya Iringa.
Green City ilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu
ya Gaddafi mabao 9-0 wakati washindi wa pili Savannah ilifanikiwa
kuingia fainali kwa kuifunga timu ya White Star ya Mbeya mabao 5-3.
Katika
mchezo huo wa fainali magoli ya Green City yalifungwa na Issa Nelson
aliyefunga magoli 3 Castro Litongwale aliyefunga magoli 3 na Lambert
Lameck aliyefunga magoli 2.
Magoli ya Savannah yalifungwa na Enhard Mgeni magoli 2 na Johnson Ngogo Aliyefunga bao 1.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi Meneja mauzo wa bia ya Castle
Lager Nyanda za Juu Kusini Vivianus Rwezaura alisema kuwa atatoa
ushirikiano wa hali na mali kwa washindi ili wafanikiwe kuwa mabingwa wa
Castle Lager Perfect 6.
Naye
Meneja wa Bia ya Castle Lager Kabula Nshimo alisema kuwa mashindano
hayo yameleta changamoto kwa washiriki na kwamba ana imani ushiriki wa
timu hizo umeongeza ari kwa vijana kupenda soka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...