Kituo cha uchunguzi na mafunzo ya magonjwa ya saratani, matumbo na ini Ukanda wa Afrika Mashariki kimefunguliwa rasmi mwishoni mwa juma. Sherehe hizo zilifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwishoni mwa juma ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Fuatilia katika picha matukio wakati wa ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipongezana na Profesa Meinrad Classen wa Chama cha Madaktari wa Matibabu ya Mfumo wa Chakula ya Ujerumani ambaye alisaidia kutafuta fedha za kujenga na kuweka vifaa tiba vya kituo hicho kutoka Kampuni ua Else Kroner Fresenius ya nchini Ujerumani baada ya kufungua rasmi kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kufungua kituo hicho.
Dkt. John Rwegasha, Bingwa wa Magonjwa ya Matumbo na Ini akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Rais, Dkt. Bilal
Dkt. Edwin Masue Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani akitoa maelezo kwa Dkt. Bilal kuhusu matumizi ya kifaa cha kufanyia uchunguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...