Kocha wa Uholanzi Louis van Gallakimpongeza Arjen Robben kwa kufanyiwa rafu iliyozaa penati na hatimaye bao la ushindi dhidi ya Mexico leo
Na Sultani Kipingo
wa Globu ya Jamii
Yaani huko Old Trafford katika klabu ya Manchester United nchini Uingereza atakoenda
kufundisha msimu ujao tayari waliishaanza kuandaa ofisi ya meneja wao mpya
Louis van Gall anayeifundisha timu ya Uholanzi katika kombe la dunia, baada ya
kuhisiwa kuwa ataaga mashindani hayo Jumapili hii walipocheza na Mexico.
Unaambiwa hadi zikiwa zimesalia dakika tatu
mchezo uishe, Uholanzi walikuwa bado wako nyuma kwa bao 1-0, huku kila mtu
akiamini kuwa bao la kipimndi cha pili la Mexico lillofungwa na Giovanni Dos Santos
limewamaliza.
Lakini baada ya kazi za ziada za kipa wa
Mexico Guillermo Ochoa kuzuia Uholanzo wasilete madhara, Uholanzi ambao
michuano iliyopita mwaka 2010 huko Afrika ya Kusini walifia fainali, wakapiga
mabao mawili ya haraka haraka na kuwaacha Mexico hoi.
Kwanza ilikuwa ni Wesley Sneijder aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 kufuatia
mpira wa kona uliomdondondokea akiwa katika mkao wa kula.
Ndipo katika dakika
ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji,
Arjen Robben aliangika chini baada ya kuchezewa rafu ndani ya 18.
Wakati huo, tayari Robben alishakataliwa
penati ya wazimkatika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na Mexico, na bila
shaka safari hii alihisi anadaiwa kitu. Kwa vyovyote vile, Klaas Jan Huntelaar
aliyeingia badala ya Robin van Persie ambaye ngoma leo ilimkataa, alifunga kwa
mkwaju wa chini kuipa Uholanzi tiketi ya robo fainali.
Dakika ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji Arjen Robben anafanyiwa madhambi
Wesley Sneijder aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 akifurahia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...