Colombia imepeleka mashabiki
wake wanaovutia kwa ushangiliaji wao hadi kwenye robo fainali za kombe la Dunia
baada ya nyota wake James Rodriguez akifunga mabao yote. Colombia waliifunga
Uruguay ya mng’ata meno Suarez bao 2-0 katika mchezo wao wa raundi ya 16 kweny
uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro jana.
Angalia goli la mwaka la Rodriguez
ambalo ni tamu sana kiasi hata huchoki kuangalia. Huku goli la adui likiwa
nyuma yake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 kwanza aliweka gambani pasi aliyoletewa, halafu kabla mpira haujatua
ardhini aligeuka na kupiga bao dakika ya 28, akiwa nje ya 18.
Hebu cheki mwenyewe. Mambo
kama haya ni marehemu Edward Chumilla tu aliyeweza kuyafanya hapa nyumbani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...