Bondia Julius Kisarawe (kushoto) leo jioni anategemea kupanda ulingoni kuzipiga na Hassan Kiwale "Morobest" (kulia) katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es salaam katika pambano la raundi nane. Muandaaji wa mpambano huo Sempai Gola na ofisa wa ngumi za kulipwa nchini Pembe Ndava walisema maandalizi yote yapo kamili, na mabondia wapo katika hali nzuri ukiondoa kasoro ndogo iliojitokeza kwa Morobest aliyekuwa acheze na Fadhili Majia na sasa atacheza na Julias Thomas Kisarawe ambae ni mbadala mkali kwani  hajapoteza mchezo katika michezo yake 12  aliyocheza. Mpambano unategemewa kuanza jioni mida ya saa kumi na kutakuwepo na mapambano mengi mno ya utangulizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...