Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania
– TRL unafuraha kuwataarifu abiria wote
na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na
kukamilika ukarabati wa daraja eneo la bonde la mto Ruvu mkoani Pwani huduma ya
treni ya abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne Juni 24, 2014 kutoka Stesheni
ya Dar es Salaam saa 11 jioni. Wananchi wanotaka kusafiri wafike stesheni zilizo
karibu yao kwa ajili ya kukata tiketi kuanzia
Juni 19, 2014.
Halikadhalika
muda wa kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya Dar
kwenda Kigoma na Mwanza utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka Kigoma na Mwanza
kuja Dar katika siku za Alhamis na
Jumapili ni saa 11 jioni kutokea Kigoma
na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.
Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake.
Uongozi wa TRL unawapongeza wananchi
kwa ujumula kwa ushirikiano na uvumilivu waliouonesha wakati wakisubiri kukamilika
kwa kazi ukarabati wa njia ya reli.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya
TRL kwa Niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Juni 18, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...