Viongozi wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, wakipanda mti wakati wa Uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyoambatana na utoaji wa Msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kutunza mazingra katika Shule ya Sekondari Miono na Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kevin William na Alex Mode wa Shule ya Kikaro wakichuana kuwania mpira baada ya kupokea msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya uliotolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mwantumu Mahiza kulia akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Alex Mode, mbuzi aliyetolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo. Miono Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya  Kikaro wakiwa wamembeba juu juu mbuzi waliopewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo baada ya kuifunga timu ya Shule ya Sekondari Miono kampuni hiyo pia imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo.
Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Said Said kulia akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuelimisha wanafunzi jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kurevya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Miono, Ally Miango shuleni hapo juzi.
Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Adam Kasale, kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa vya michezo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Gabriel Dominc baada ya Kampuni hiyo kutoa msaada kwa shule hiyo na Miono zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe Mwamtumu Mahiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...