JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.
Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.

Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz  na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tzna watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI
http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf
http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf

Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza
baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.

Sgn Isaac J. Nantanga

MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2014

    Ni wazi hali si shwari na majirani zetu Tanzania, Adui anaweza kabisa kujipenyeza kwenye Michakato kama hii.

    Muwapekue vya kutosha hao Maafisa wa Uhamiaji watarajiwa msije mkasajili Mabanyamulenge wa Rwanda na Mabwenga wa Kiganda (WAKAWA MAAJENTI WA KIKACHERO WAKILIPWA KUTOKA KIGALI NA KAMPALA) baadaye tukaja kujilaumu wenyewe!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2014

    Hata ndugu zetu wa hapa hapa wanaweza wakaacha uzalendo na kusahau mchakato waliopitia wakashindwa kufuata maadili wanapopewa chochote.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2014

    Michuzi, nakuomba sana uangalie ni aina gani ya ujumbe unauweka katika blog yako. Ni jukumu letu sote kuilinda jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...