![]() |
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii. |
![]() |
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
![]() |
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru. |
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa Mujibu wa Mh Nassari
,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote
wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la
Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna
kadi.
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.
Nassari amesema watu zaidi
ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake
wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali
.
Ooooppss! warning ,bachelor expiring but hassles and puzzles will exist soon! Get ready for that.
ReplyDeleteMungu aimarishe uhusiano wenu ndoa ipate kudumu. Mtangulizeni Mungu na kwa uhakika ndoa ita dumu. Maisha ya ndoa yanadumu.mkishirikiana. Maisha ya ndoa yanadumu msipokuwa na siri na kubwa kuliko vyote mkimtanguliza Mungu kama Nuru yenu upendo wenu utadumu na kuongezeka. Nawatakia kila la kheri na kuwaombea ndoa ya kudumu na yenye mafanikio. Hongera sana.
ReplyDeleteBachelor Expiring???
ReplyDeleteJamani haya makubwa tena. Kweli lugha sio yetu, kama hatuifahamu, tusijilazimishe.
ongera Nassari
ReplyDelete