Mh. Zitto Kabwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2014

    mawazo ni mazuri; wahusika waangalie

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2014

    Nafikiri ni ruksa kuijadili hii hoja licha ya kutegemea majibu murua kutoka kwa Mh. Saada.

    Hoja zako ni nzuri na zenye kufanyiwa utafiti, ila katika nafasi hii finyu naomba kutofautiana na Mh. Zitto kuiruhusu mifuko ya jamii kuingia kwa biashara ya kutoa mikopo. Fedha za wanachama wa mifuko ni hazina zao za kipindi hicho amabacho watakuwa hawana nguvu na misuli ya kuifukuza shilingi, hivyo ni fedha ambazo zinatakiwa ziwekezwe kwa umakini wa hali ya juu. Kutoa mikopo nafikiri mnajua ilivyo "risky business". Mpaka benki zinaambiwa sio rafiki wa mtu asiye na pesa (situmii neno "maskini" kwa makusudi), ni kwa sababu ya athari zilizopo kwa watu au biashara kama hizi. Na hii ni dunia nzima pamoja ya kwamba Afrika tumezidi kidogo. Nchi kama Marekani wana kitu kinaitwa SBA (Small Business Administartion) kwa ajili ya kusaidia biashara ndogondogo. Naelewa woga wa kuanzisha kitu kama hicho hapa kwetu (ufisadi). Hakika ufisadi ni doa moja kubwa kwa ustawi wa jamii!!

    Benki inabidi ziwekewe ukomo wa kununua dhamana za serikali ili zishiriki katika kuwa creative ili kukopesha pesa zao kwenye sekta za uzalishaji (real sectors). (mmesikia walichoambiwa benki za eurozone na ECB).

    Sikubaliani na hoja ya serikali kutoa mchango kwa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kila mwanachama mkulima anayechangia, kwani hapo ni matumizi mabaya ya fedha hadimu za kodi. Wakulima wapewe ujuzi, mbegu bora na miundombinu ya barabara na masoko, pamoja na "financial Education", wataweza kujiwekea akiba vizuri tu. Mazao yetu bado yana soko kubwa mno(organic products), mkulima alindwe kwa kuzuia vitu kama GMO (genetically modified organisms) maana hilo ndilo tishio kubwa la maisha ya mkulima pamoja na afya ya mlaji, uharibifu wa ardhi, maji na hewa, na udhalilifu wa uoto wa asili (maana hata nyuki na vipepeo wanaathirika na GMO).

    Mh. Zitto naona umesahau umuhimu wa kuongeza ujuzi kwa nguvukazi ya taifa letu. Hapa ndipo watu watakapokuwa na uwezo wa kujitegemea (self-reliance) na kuacha kuwa mzigo!

    Kodi kwa wafanyakazi: mbona hili liko wazi mno? Hivi hawakuelewi kwa hizo takwimu unazotoa? Mh. Saada, ebu wapunguzie mzigo wavuja-jasho wafanyakazi!!

    Kurasimisha biashara na kuandikisha walipa kodi: Sio tu daftari la wapiga kura linatakiwa kuboreshwa, na walipa kodi waandikishwe! La sivyo itakuwa ni kuwatesa wale wachache walioandikishwa.

    Ongezeko la uchumi chini ya asilimia 9 haliwezi kuleta neema nchini. Wachumi wanasema ili kuwe na "impact" uchumi inatakiwa ukue sio chini ya mara tatu ya asilimia ya ongezeko la watu! Hivyo Waheshimiwa Wabunge, msishangilie hata kidogo hizo asilimia za kukua kwa uchumi zinazotangazwa na serikali, bado tuko shimoni!!

    Mh. Zitto endeleza mapambano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...