Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy,Brian Tracy kutoka nchini Marekani,akizungumza jambo mapema leo asubuhi katika moja ya ukumbi wa Serena Hotel,jijini Dar kuhusiana na semina maalum ya uongozi bora ilioandaliwa na Mikono Speakers iliyomuhusisha nguli huyo wa masuala ya uongozi na kutoka nchini Marekani na Azim Jamal pichani kulia ambaye ni  mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.Wa pili kutoka kulia  ni Wakurugenzi wa Mikono Speakers ambao ndio waandaji wa semina hiyo maalum ya Uongozi na kushoto ni  (Deogratius Kilawe na Themi Rwegasira.

====== ======  ======= 
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Mikono Speakers wanakuletea semina maalum ya Ufanisi bora katika Uongozi itakayoongozwa na Nguli wa masuala ya uongozi na maendeleo, Brian Tracy kutoka nchini Marekani na Azim Jamal kutoka nchini Canada. Semina hii maalum chini ya nguli hao wenye kuheshimika duniani ni fursa ya kipekee kwa wa-Tanzania kujifunza na kuboresha vipaji vyao vya uongozi katika biashara na taasisi zao mbalimbali. Semina hii ya siku moja itafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam tarehe 13 ya Mwezi Juni, 2014.

Akiongelea kuhusu umuhimu wa Semina hii kwa umma wa Tanzania, mkurugenzi mkuu wa Mikono Speakers, ndugu Deogratius Kilawe aligusia kuhusu kukosekana kwa wa-Tanzania katika eneo la juu, hususani katika nyanja ya uongozi. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...