Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo asubuhi hii wakati wa seina inayojadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio ya mfuko huo, malengo na Changamoto zake katika kufanikisha huduma ya afya kwa jamii, ambapo uwigo wa walengwa katika huduma hizo umeongezeka kutoka kaya 120 mwaka 2009 na kufikia kaya 668.474 mwaka 2014 sawa na wanufaika milioni 4.01 na mpaka sasa mfuko huo unafanya kazi na Halmashauri za wilaya 129 katika nchi nzima kati ya Halmashauri 168 zilizopo lakini pia tayari Halmashauri 20 kati ya hizo zimeshahamasishwa na zitaingia katika mpango huo siyo muda mrefu, .(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-BAGAMOYO)
Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji akitoa mada katika semina hiyo juu ya uchangiaji wa huduma za mfuko wa bima ya afya kulia ni Raphael Mwamoto Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti na katikati ni Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF) 


Dk Frank Lekey Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Kitaaluma akitoa mada kuhusu uboreshaji wa huduma za mfuko wa Afya ya jamii ambapo kwa sasa wanafanya kazi na hospitali za serikali na baadhi ya hospitali za mashirika ya dini.
Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF) akizungumzia mafanikio yaliyokwishapatikana kutokana na huduma za mfuko wa Afya ya jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...