JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI

TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad Wilson Ngewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.
Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria
ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini
Tanzania.
Imetolewa
na:
Katibu Mkuu
Wizara ya
Uchukuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...