Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kutetereka kwa  mojawapo ya madaraja katika bonde la mto Ruvu katika  reli ya kati , umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa  daraja utakapokamilika.

Hapo jana  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi Mchundo Ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini ili kuona uharibifu uliotokea na mahitaji kuliimarisha ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji, ukarabati wa kulirejesha katika hali ya kutumika utachukua takriban wiki moja na hivyo kuanzia jana saa 12 jioni eneo la reli kati ya Dar es Salaam na kilomita 82/5 Ruvu limesitishwa kwa huduma za usafiri wa reli.

Kwa taarifa hii  wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla  ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya jana ya  Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala. Wakati taarifa hii inatolewa katika vyombo vya habari zoezi la kuwarejeshea nauli abiria wapatao 1000 lilikuwa zinaendelea   katika stesheni mbali mbali za TRL na hasa katika Stesheni  kubwa ya Dar es Salaam ambapo safari kwenda bara huanzia.

 Aidha Uongozi wa TRL umeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Juni 11, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...