Mubelwa Bandio akimhoji Fabian Lwamba wa KRYSTAAL

Katika NJE-NDANI wiki hii kati ya utakayosikia mahojiano na Fabian Lwamba Mmoja wa ndugu watatu wanaounda kundi la KRYSTAAL ambao walizaliwa kwenye familia iliyojiweza, lakini mgogoro wa kisiasa ukawafanya waikimbie Zaire na kutengana.
Michael, Fabian na Alistone Lwamba wanaounda kundi la KRYSTAAL
Walikuja kuungana Canada ambako kwa miaka 16 wamekuwa pamoja kama kundi la muziki wa injili
Wametoa albamu 6 na kupata tuzo 26
Pia utamsikia ripota wetu Sebastian Atilio ambaye amerejea kutoka safari ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Sebastian Atilio na wenzake wakiwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro
Aliona nini huko? Alijifunza nini? Ni kipi alichogundua kama udhaifu mkubwa kwenye rasilimali zetu huko?
Yote haya na mengine mengi ni kwenye NJE-NDANI na Mubelwa Bandio, Jumamosi kuanzia saa 6 kamili kwa saa za Marekani mashariki (NOON EST) kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...