JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.

Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.

Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.

Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.

Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz  na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tz na watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.

Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.

Sgn
Isaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

18 Juni, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2014

    Interview ya zaidi ya watu 1000 Kazi kwenu. Ingekuwa ofisini kwetu...Mbinu za kisasa za kushort list online applicants zinatumika kwa kutumia key words zinazotokana na vacancy announcement. Katika maelfu ya waombaji computer inachuja wale waliondika relevant information kwenye covering note na kutema wengine wote. Written test ingekuwa kwa ajili ya applicants kati ya 210-250 (70 X3)... Oral interview ingefanywa kwa watu kati ya 140-150 tu..ili upate watu 70 unaowataka.

    Hili zoezi limethibitisha kuwa katika Afrika na hapa nchini private sector inatakiwa kukua kwa kasi ili ajira ziongezeke.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2014

    Msafara wa Mamba Kenge hawakosekani!

    Idadi hiyo kubwa ya watu 1000 wasiwasi wangu wasije wakajipenyeza Mawakala wa Kagame hapo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2014

    Mdau wa Kwanza hiyo Teknolojia yenu ya kisasa ya Uchujaji Waombaji wa kzai inawakosesha wengi Fursa!

    Ni bora mkafanya 'Manually' zaidi ya 'Diditally' hizi ni Nafasi za Serikali na kwa ajili ya nchi na wananchi, kwa kuwa miongoni mwa mtakao watema inawezekana tukamkosa Afisa mahiri wa Mamlaka kwa miaka ijayo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2014

    Ahhh Mdau wa kwanza hiyo Sayansi yako inakosesha watu wanaostahili na wenye sifa kazi, matokeo yake itachagua watu 'Vihiyo'!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2014

    Mwanasayansi Albert Einstein aliwahi kuandika mawazo haya ''I fear the day when mankind will be too much depending on technology'' akimaanisha ya kuwa 'NINAOGOPA ITAKAPO FIKA SIKU BINAADAMU AKIWA ANATEGEMA SANA TEKINOLOJIA KTK MAMBO YAKE' hapa ana maana utegemezi sanma wa Tekinolojia una makosa na madhara yake makubwa:

    Mfano hiyo njia ya kutumia Tekinolojia ya kisasa ya kuchambua waombajiwa kazi inaweza kuchagua wasio Stahili na wasio na sifa ikaacha wenye sifa na wanaostahili!...(TEKINOLOJIA PEKEE HAIAMINIKI KAZI YA BINADAMU NI MUHIMU KUHAKIKI KAMA SAYANSI AMA TEKINOLOJIA INAFANYA KAZI SAHIHI) HUO WASI WASI WA MWANASAYANSI ALBERT EINSTEIN KUNAKO KARNE YA 18 HADI 19 HUKO UNAKUJA KWA MANTIKI HIYO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2014

    Hii teknolojia inatumika kwenye kazi za umoja wa mataifa kwa wale wanaoapply kutumia system ya inspira, kwenye UN Careers portal..human intervention inakuja baadaye. Waati wa Albert Eisten computer hazikuwepo applicants walikuwa wachache. Reality Check kuinterview watu watano ni kazi ndio sembuse 1000 utaweza tu uki-outsource au kutumia muda wa kazi za kawaida kwa ajili ya kusaili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...