Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wizara ya Uchukuzi, Bw.
Issa Nchasi, akifanya usafi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam kama sehemu ya
maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza
mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake wakiwa kwenye
zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho
ya siku ya Mazingiza Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi,
Tumpe Mwaijande (kulia), akipanda mti katika eneo la bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi,
kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira. Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira
yanafanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’.
(Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...