TAKRIBANI watu 17 wamepoteza maisha  na wengine  56  kujeruhiwa baada ya basi la la Morobest lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma leo. 
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Said Lusogo liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na dereva Gilbert Isata Nemaya.
 Amesema atika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha, ikiwa ni wanaume 12 na wanawake watano Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga basi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...