Wafanyakazi wa kampuni ya Majembe
Auction Mart wakifungua mashine ya kutengenezea matofali katika eneo la Kwa
Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam.Wizara ya Maji iliamrisha kukamatwa kwa vifaa na mali mbalimbali za
Martin Kessy aliyekuwa amejiunganishia maji kinyume na sheria na kufanya
biashara ya kufyatua matofali. Zoezi
hilo linaendelea. Zoezi hilo limefanyika jana katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam jana. .
Mwenyekiti wa kamati maalum ya Wizara
ya Maji, Eng. Hamis Blangson (kulia) akisikiliza jambo wakati wa operesheni
maalum ya kupambana na watu wanaojiunganishia maji kinyume na sheria na
kusababisha hasara kwa serikali na matatizo ya huduma hiyo kwa wananchi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Bw. Twaha Mohamed (kushoto) na Bw. Juma Maingu (katikati). Zoezi hilo linaendelea
Kifaa cha kubebea vifaa vizito cha
DAWASA kikiondoka na moja ya mashine ya kutengenezea kutengenezea matofali
katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam.
The mdudu zee la kuona mbali,kwa mpangu huu ule mpango wa MATEKEO MAKUBWA SASA utafanya mambo yaende mswano kazeti buti maana mlilala mno ndio maana wanakuchezeeni kama vifaranga vya kuku.
ReplyDeleteHebu waachieni watu wajiungie wenyewe mana mtu akitaka huduma atazungushwa wee mpaka atachoka
ReplyDeleteDuhhh!
ReplyDeleteHuu ni Uhandisi uliotukuka kwa mtu kuishia Darasa la Pili Shule ya Msingi halafu akajifungia mwenyewe mtambo wa kusukumia maji!
Hapa ndio utaamini kuwa Watanzania huwa tunzazaliwa tukiwa tayari tumesha elimika!
Tungekuwa tuna utendaji wa namna hii kila idara Serikalini nadhani hata Raisi Jakaya Kikwete angalau na yeye angepumzika!
ReplyDeleteAu jamaa Kijogoo (aliye jiunganishia maji mwenyewe) aliwaruka Dwasco kuwapa chao?
ReplyDeleteNadhani ndio maana nao wakamzignua !!!
Ohhh, Tanzania imekuwa ni Italia ya pili?
ReplyDeleteKule ktk Italia maeneo ya Miji ya Kusini pana magenge ya Makundi ya Umafia yanamiliki kwa kuzishikilia huduma za maji na umeme kama idara za serikali!
Haya mambo ya kudhibiti huduma za maji na umeme kwa makundi ya Kijambazi yapo Italia.