Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa na wajibu na jukumu kubwa la kuwatunza na kuwathamini wazee wasiojiweza hivi sasa kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa kwa nchi hii wakati wa kulitumikia Taifa lao. 
Alisema mchango wa wazee hao umekuwa ukiendelea kutumiwa na wananchi walio wengi hapa nchini ikiwemo kigezo cha amani na utulivu kinachotokana na juhudi za wazee hao wakati wa kupigania utu wa mwafrika.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa ziara yake fupi ya kuwasalimia Wazee wanaotunzwa katika Nyumba za Serikali za Welezo na Sebleni na kuwapatia zawadi ya nguo kwa ajili ya kusherehekea vyema siku Kuu ya Iddi El Fitri inayotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo. 
Alisema wazee wa Taifa hili wametumia muda wao mkubwa wa kujenga mazingira bora ili kizazi chao kiendelee kuishi kwa amani na furaha tofauti na enzi zao zilizokumbwa na mitihani ya kutawaliwa jambo ambalo liliwakosesha uhuru wa kidemokrasia wa kufanya wanalolihitaji katika maisha yao. 
Akitoa skurani kwa niaba ya wazee hao wa Welezo na Sebleni Mzee Omar Said alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa juhudi zake za kuendelea kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao juhudi ambazo zimekuwa zikiwapa faraja wazee hao na kuendelea kujenga imani kwa Serikali ambayo inaelewa mchango wao katika ukombozi wa Visiwa hivi. 
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Bibi Asha Abdulla alisema Nyumba za Wazee ziliopo Welezo zimekuwa zikihudumia wazee wapatao 42 wakati zile la Sebleni zinahudumia wazee 46 wakiwa chini ya usimamizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii iliyopewa jukumu la kuwahudumia wazee hao.
 Baadhi ya Wazee wa nyumba za Serikali za Welezo wakifutilia maelezo ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alipowatembelea kwenye makazi yao.
 Balozi Seif akigawa zawadi kwa mmoja wa wazee wa Welezo alipowatembelea na kuwafariji wakiwa ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
 Balozi Seif akimkabidhi zawadi mmoja wa watumishi wa wazee wanaoishi katika nyumba za Serikali zilizopo Welezo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya Wazee wa nyumba za Sebleni wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akijiandaa kuwapatia zawadi kwa ajili ya siku kuu ya Iddi el Fitri.

 Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya wazee wa kike wanaotunzwa katika nyumba za Serikali zilizopo Sebleni Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa zawadi kwa Wazee wa kiume wa Sebleni
Mzee Omar Said wa Nyumba za Sebleni kwa niaba ya wazee wenzake wa Sebleni na Welezo akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hayupo pichani kwa juhudi zake za kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao.
Picha na Hassan Issa wa  OMPR 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...